@bishop_geography_ ametangaza kuwa TAREHE 10 mwezi Wa SABA Katika Kanisa la Ufunuo Morogoro kutakuwa na Sherehe ya wamama wa Ufunuo pamoja na Kusherekea Miaka 8 tangu kanisa hilo lianzishwe.
Kupitia Instagram account ya @bishop_geography_ amethibitisha kwamba Irene Uwoya ndio atakuwa Mgeni Rasmi katika Sherehe hiyo.
"Wamama ni jeshi kubwaaaa, Jumapili hii wamama wa Ufunuo Morogoro, wana jambo Lao, wakiwa na mwanamama mchapa kazi, mjasiriamali, super women @ireneuwoya8, mwanamke imara ni yule mwenye uchumi imara, woooote mnakalibishwa, Tutakula chakula pamoja, MUNGU HAJAWAHI KUSHINDWA-@bishop_geography_
Poster inayoonesha kuwa Irene Uwoya atakuwa Mgeni Rasmi katika tukio hilo la Kanisa inatembea sana WhatsApp Status huku wengi wakitoa Maneno ya Kejeli kuhusu uteuzi huo.
Vipi una maoni gani? Irene Uwoya amestahili kupewa Ugeni Rasmi katika Tukio hilo la Kanisa au Hajastahili?