Jana ilikuwa kumbukumbu ya siku ya kuzaliwa ya @mama_dangote , watu mbalimbali hasa familia ya WCB walimpost mama dangote huku wakisindikiza Caption nzuri za kumtakia Mafanikio mengi mno.
@officialzuchu pia aliona sio mbaya akaamua ampost mama mkwe wake, na akaandika:
"Happy birthday mamaa
Kamanda Allah Akupe furaha na Afya Na Kila hitaji la Maisha yako 🥰🥰 @mama_dangote"
Baada ya Kupost post hiyo kuna mtu mmoja alicomment kwamba "Akikujibu niite Mbwa", kama utani vile mpaka sasa mama Dangote bado hajacomment chochote kwenye ile post, zaidi ameirepost post hiyo kwenye Insta Story tena kishingo upande.
Ili kujiridhisha zaidi niliamua kutembelea page za watu mbalimbali waliompost mama Dangote, nikagundua kwamba alikuwa akicomment katika hizo post, mfano Romy Jones alimuwish na Mama Dangote akacomment.
Je kwanini ameshindwa kukoment kwa Zuchu na akaamua tu kurepost kwenye Insta Story, je wana ugomvi? Je mama dangote hapendi ukaribu wa Zuchu na Diamond? Kama kweli Zuchu na Diamond ni wapenzi inamaana mama dangote hautaki huo uhusiano? Hapa kuna kitu kimejificha, yajayo yanafurahisha.