Baada ya picha ya @officialnandy akiwa na Mimba kuzagaa sana Mitandaoni huku watu wengi wakimpongeza, Mwanamtandao maarufu @mwijaku yeye yupo tofauti na watu wengi wala hajaona haja ya kumpongeza Bill wala Nandy.
Mwijaku amefunguka kwamba sio jambo jema mwanamke kupata mimba nje ya ndoa na hata tukirudi katika suala la Dini tunaona kabisa ni makosa makubwa sana kupata mimba nje ya Ndoa.
Kiukweli nasimama na Mwijaku, maana ukiangalia katika Uisilamu na Ukristo hakuna dini ambayo imeruhusu watu wafanye mapenzi/ kupata mimba kabla ya Ndoa, sasa Nandy na Billnass wamekosea Mno.
Hii ni aibu hasa kwa nandy kwani hana tofauti na watoto wa Secondary ambao huwa wanapata mimba. Pia sizani kama wazazi wa nandy wamelichukulia Suala hili vizuri maana Nandy Amezini sana na Billnass mpaka amepata mimba, ni kosa kubwa Kidini.