Klabu ya dodoma jiji imemtambulisha mchezaji wao mpya Randy bangala ambae ni mdogo wa kiungo wa klabu ya yanga yannick bangala kuitumikia timu hiyo msimu huu wa ligi kuu ya NBC.
Tayari klabu hiyo imewatangaza wachezaji wawili raia wa ghana ambao msimu uliopita waliichezea klabu ya Biashara United ya mara ambayo imeshuka daraja
klabu hiyo tayari imemtambulisha kiungo christian zigar pamoja na Collins Opare ambaye hucheza nafasi ya mshambuliaji
Randy bangala mara ya mwisho aliichezea timu ya TP Les Croyant ya DRC, FC Renaissance,jeunesse sportin Tsangu na AS Maniema Union za DRC