HARMONIZE AWAPIKU BURNABOY NA ED SHERAN


 Katika Album ya BurnaBoy iliyotoka Rasmi Jana, hapo hapo aliachia Video ya kwanza kutoka katika Album hiyo. VIDEO YA FOR MY HAND, Wimbo namba 13 kati ya 19 zinazopatikana katika Album yake, Wimbo huo amemshirikisha Ed Sheeran.


Mpaka sasa Wimbo huo pande za Youtube una Views Million 1.5 huku Deka ya Harmonize iliyoachiwa masaa Matano mbele yake ina zaidi ya Views Million 2.9.


Hivyo kwa akili ya kawaida utasema kwamba Deka ya Harmonize imeifunika Views For My Hand.


Lakini aliyeturoga wabongo ni nani? maana sisi tunaamini kwamba Msanii mkubwa anapatikana youtube wakati wenzetu msanii mkubwa anapatikana SPOTIFY, APPLE MUSIC, TIDAL, AMAZON N.K. Ifike wakati tuwekeze nguvu zaidi katika mitandao hiyo, youtube hakuna Deal, hata Chikumbalaga anaweza kuachia ngoma na ikapata Views Million 100.


Masaa 16 yaliyopita Page maalumu ya @billboard imepost Cover ya Album ya BurnaBoy, hivyo tutegemee lolote Ngoma kama For My Hand inaweza kupenya muda wowote kwenye Chart za Billboard.



Post a Comment

Previous Post Next Post