Kupitia katika Kipindi cha Amplifier (Clouds Fm) Mtangazaji Millard ayo amekiri kumkubali sana msanii Tems. Kumkubali huko sio kumkubali kikawaida, nadhani wakubwa mnaelewa.
Millard akaendelea kusema kwamba hata ikitokea Tems amuite hivi sasa basi Millard yuko tayari kuacha mishe zake chap na akamfata Tems alipo. Millard anateswa kihisia na Tems kama ambavyo Rema pia anateswa maana yeye kaamua kabisa kuweka Picha ya Tems kwenye Dp yake Twitter.
Lakini hili jambo Meena Ally amelipokeaje? Maana mara kadhaa watu hawa wamekuwa wakihisiwa kuwa wapo kwenye uhusiano fulani hivi lakini haijawahi kuthibitishwa maana wote ni wakimya mno hawapendi Show Off, lakini ukichunguza kwa ndani zaidi utagundua kwamba Meena Ally huwa kuna muda anashindwa kuzuia hisia zake kwa Millard, sasa lolote linaweza kutokea kuanzia sasa maana Ayo kashachafua hali ya hewa.